Viongozi wa kundi la MRC wamelalamika kuhangaishwa na polisi

Viongozi wa kundi la MRC wamelalamika kuhangaishwa na polisi

Viongozi wa kundi la Mombasa Republican Council (MRC), wamelalamikia hatua ya kuhangaishwa na kukamatwa kiholela na maafisa wa polisi licha ya Mahakama kuu nchini kuhalalisha kundi hilo.

Wakizungumza na vyombo vya habari, viongozi wa kundi hilo wakiongozwa na Frankline Gumbo wanadai wamekuwa wakihangaishwa na serikali licha ya kutii agizo la Mahakama la kuwataka kutekeleza shughuli zao kihalali bila kujihusisha na visa vya uhalifu.

Gumbo alibainisha kuwa hatua hiyo inaendelea kuzua hofu miongoni mwa wanachama wake hali mbayo imechangia kupungua kwa kiasi kikubwa idadi ya wanachama wa kundi hilo.

INSERT: MRC KUHANGAISHWA

Wakati huo huo, Gumbo amedokeza kwamba kundi hilo limekuwa likiendeleza shughuli zake za kutafuta usaidizi kutoka miungano na mashirika mbali mbali ili kupata msaada wa kutekeleza malengo yake pasi na kuzua vurugu ama taharuki.