Mapato ya kilimo cha mboga na matunda yalipungua hadi shilingi bilioni 136.6 ikilinganishwa na shilingi bilioni 156.7 zilizonakiliwa mwaka jana.
Mapato ya majani chani pia yalipungua kwa asilimia 84 hadi shilingi bilioni 178 katika kipindi hicho.
Washikadau katika sekta ya kilimo walisema huenda hali ikawa mbaya zaidi iwapo wakulima hawataafikia viwango vya kimataifa vinavohitajika.
Taasisi za kifedha zilitakiwa kutoa mikopo kwa wakulima wa viwango vya chini kununua pembejeo ambazo zinawasaidia kuafikia viwango hivyo.
Mkurugenzi wa viwango katika kampuni ya Trade Market Afrika Andrew Edewa alisema vyeti vingi vya kimataifa huwa ghali kupata hivyo ipo haja ya kufadhili wakulima zaidi ili kuhakikisha bidhaa nyingi za humu nchini zinauzwa katika masoko ya nje.
Wakati huo huo wakulima walishauriwa kubuni vyama vya ushirika ambavyo vitawawezesha kupata mikopo ya riba nafuu.
Taarifa ya Pauline Mwango
