EPRA kutoa elimu kuhusu kanuni mpya za mpango wa nishati wa 2025

EPRA kutoa elimu kuhusu kanuni mpya za mpango wa nishati wa 2025

Mamlaka ya udhibiti wa kawi na petroli (EPRA) imekutana na maafisa wa Serikali ya Kaunti ya Mombasa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu kanuni mpya za mpango jumuishi wa nishati kitaifa wa mwaka 2025.

Kanuni hizo zinaelekeza uandaaji wa mipango ya nishati kulingana na mahitaji ya wananchi katika ngazi ya kitaifa na kaunti.

Mtaalamu wa mipango ya nishati kutoka EPRA, Raymond Asungose alisema mpango huo unahusisha ukusanyaji wa taarifa kutoka kwa wananchi ili kusaidia kupanga miradi ya nishati kwa usahihi.

Aliongeza kuwa mpango huo utasaidia kaunti kuwa na msingi thabiti wa kuandaa bajeti ya miradi ya nishati kila mwaka, na hivyo kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa serikali za kaunti.

Kwa mujibu wa EPRA, kaunti zote 47 zinatarajiwa kushirikishwa katika mchakato huu kabla ya mwisho wa mwaka wa kifedha ifikapo Juni 2026.

Taarifa ya Mwanahabari wetu