Wafanyabishara Kilifi walalamikia gharama ya maisha

Wafanyabishara Kilifi walalamikia gharama ya maisha

Wafanyibiashara humu nchini wanaendelea kulalamikia kudorora kwa uchumi siku chache tu baada ya rais Wiliam Ruto kusema kuwa uchumi wan chi umeimarika.

Wakizungumza mjini Kilifi kaunti ya Kilifi wafanyibiashara wanaojihusisha na biashara za kuuza mbonga wamesema kuwa wateja wamepunguza kiwango cha bidhaa wanazonunua kutokana na hali ngumu ya maisha.

Aidha waliongeza kuwa bidhaa nyingi sokoni zimepanda bei kutokana na gharama ya juu ya uzalishaji.

Waliitaka serikali kupunguza gharama ya maisha pamoja na kuwawezesha na fedha za mikopo ili kujiendeleza kimaisha.

Wakati huo huo waliitaka serikali kuu na kaunti ya Kilifi kuwawezesha wakulima na mbinu za kisasa za kilimo ili kuongeza mapato ambayo yatainua uchumi wa kaunti.

Taarifa ya Pauline Mwango