Waziri wa Kilimo nchini Mutahi Kagwe amesema tangu vita kuanza katika maitaifa ya Ghuba kati ya Israeli na Marekani dhidi ya Iran, Kenya imekuwa kipata hasara ya takribani shilingi milioni 300 kila wiki.
Kagwe alisema Kenya imekuwa ikisafirisha nyama katika taifa la Iran na tangu vita hivyo vianza biashara hiyo ya kimataifa imekuwa changamoto kwani mifugo na nyama nyingi zimekuwa zikisalia kwenye mabehewa.
Waziri Kagwe alisema mji wa Dubai ambao pia umekuwa ukipokea Chai umekuwa changamoto kusafirisha biashara hiyo katika mataifa Ghuba, akisema tayari mazungumzo yameanza kuhusu suala hilo.
Adha alisema serikali imeanza kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha bidhaa za Kenya zinasafirishwa katika mataifa ya Ghuba licha ya changamoto zinazoendelea kushuhudiwa kutokana na vita vinavyoendelea Iran.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
