Wawekezaji wakuu nchini waingia katika mkataba wa kiuchumi

Wawekezaji wakuu nchini waingia katika mkataba wa kiuchumi

Benki ya KCB kwa ushirikiano na bebki ya Afrexim zimeingia kwenye mkataba wa maelewano unaolenga kutoa usaidizi wa kuwezesha kifedha na kibiashara kwa wawekezaji wanaoendesha shughuli zao katika eneo la kiuchumi la Vipingo kaunti ya Kilifi.

Chini ya makubaliano hayo benki hizo mbili zitatoa ufadhili wa dola milioni 500 na 300 za marekani mtawalia kwenye mradi huo.

Tangazo hilo lilitolewa wakati wa mkutano uliowaleta pamoja viongozi wa kibiashara mbalimbali na wawekezaji  kujadili jinsi ya kuiweka kenya katika nafasi ya kuwa kivutio kikubwa cha uwekezaji.

Akizungumza katika eneo la Vipingo kaunti ya Kilifi, Mkurungezi wa benki ya KCB Paul Russo alisema kuwa mkataba huo unaashiria hatua muhimu wa ukuaji endelevu wa viwanda nchini kenya na kukuza ufikiaji wa masoko ya kimataifa.

Kulingana na wadau wa sekta ya maswala ya uchumi hatua hiyo itawanufaisha wawekezaji kutokana na shindani ili kuanzisha shughuli zao katika eneo hilo kwa kuzingatia viwanda, mazao kutoka kilimo na biashara za kuongeza thamani.

Taarifa ya Pauline Mwango