Stanley Kenga kupeperusha bendera ya DCP-Magarini

Stanley Kenga kupeperusha bendera ya DCP-Magarini

Mwanasiasa Stanley Kenga Karisa imejiunga rasmi na Chama cha DCP kinachoongozwa na Rigathi Gachagua.

Kenga amejiunga na Chama hicho ili kugombea ubunge wa Magarini kaunti ya Kilifi utakaoandaliwa Novemba 27 mwaka huu baada ya kushurutishwa kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho kupitia chama cha UDA.,

Akizungumza baada kukabidhiwa tiketi ya DCP na Kinara wa chama hicho Rigathi Gachagua, Kenga alipongeza uamuzi wa Chama cha DCP kwa kumpa nafasi ya kugombea ubunge wa Magarini, akisema wakaazi wa Magarini wako na nafasi nyengine katika uchaguzi huo mdogo.

“Wakati milango ilipofungwa ile ng’ambo ya pili hapa DCP, mlitufungulia milango, mkatupokea na tunashukuru. Kwa sababu mmepekea nafasi kwa jamii ya Magarini tuwezekuwa kwa debe kwa huu uchaguzi mdogo ambao unakuja tarehe 27 mwezi wa Novemba, ninasema kwamba tuko tayari na tutachukua kiti cha Magarini kupitia DCP”, alisema Kenga.

Wakati huo huo aliahidi kuhakikisha Chama cha DCP kinashinda uchaguzi huo mdogo wa Magarini, huku akiwarai wafausi wake kutorudi nyuma katika kupigania demokrasia.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi