Vijana nchini wahimizwa kukumbatia kilimo bustani

Vijana nchini wahimizwa kukumbatia kilimo bustani

Vijana humu nchini wamehimizwa kukumbatia ukulima wa bustani ili kujiiinua kiuchumi.

Kulingana na Swalehe Joha ambaye anaendeleza kilimo hicho kutumia mitungi, alisema wakulima wanaweza endeleza kilimo bila hata kuwa na shamba.

Akizungumza na coco fm Joha alisema kuwa ameendelea kufaidika kupitia kilimo hicho cha bustani huku akiwata vijana hasa wanabodaboda kujihusisha na kilimo hicho ili kujinufaisha.

Aidha Joha alieleza kuwa kupitia aina ya kilimo hicho amepata faida kwani mtungi mmoja anaweza kupanda mimea 20 jambo ambalo anataja kuimarisha maisha.

Aliwashauri vijana ambao hawana ajira pamoja na wahudumu wa bodaboda kukumbatia aina hii ya kilimo ili kujiendeleza kimaisha na kukoma kulaumu serikali kutokana na uhaba wa ajira.

Taarifa ya Pauline Mwango