Rais William Ruto aikabidhi bodi ya majani chai shilingi bilioni 2.65

Rais William Ruto aikabidhi bodi ya majani chai shilingi bilioni 2.65

Rais William Ruto ameikabidhi bodi ya majani chai shilingi bilioni 2.65 zilizopatikana kwa benki ambazo zimeshindwa kujiendeleza.

Pesa hizo zilitoka kwa benki ya Chase na Benki ya emperial ambazo zilikuwa zimechukua pesa za wakulima wa majani chai kote nchini.

Kupitia shirika la bima wakulima wa majani chai watalipwa fidia ya hasara iliyosababishwa na kuporomoka kwa benki hizo.

Akizungumza na zaidi ya wakulima 600,000 wa majani chai katika ikulu ya Nairobi rais Ruto alitaka bodi ya majani chai kuhakikisha kuwa pesa hizo zinawafikia wakulima.

Kama juhudi ya serikali kuimarisha sekta hiyo rais ruto alisema kuwa bei ya majani chai imeongezeka katika kipindi cha miaka miwili kutokana na mageuzi yaliyoletwa katika sekta hiyo.

Aidha alisema mapato ya majani chai yamepanda kutoka shilingi bilioni 138 mwaka wa 2022 hadi shilingi bilioni 215 mwaka 2024, huku serikali ikilenga kufikia shilingi bilioni 280 ifikapo mwaka 2027.

Taarifa ya Pauline Mwango