News

Bunge la kitaifa kuhamasisha umma katika maonyesho ya Kilimo, Mombasa

Published

on

Bunge la kitaifa linashiriki maonyesho ya kilimo ya kimataifa ya Mombasa kwa mara ya kwanza katika historia yake, ambayo yanaanza rasmi Jumatano Septemba 3, 2025 katika uwanja wa Mkomani.

Bunge hilo limeweka banda maalum la kuhamasisha umma kuhusu majukumu na shughuli zake.

Kamati ya kikosi kazi cha bunge inayoongozwa na mwenyekiti Owino Harrison ilishinikiza wananchi kujitokeza na kujifunza kuhusu historia ya bunge, utungaji sheria na nafasi ya taasisi hiyo katika utawala wa taifa.

Owino alisema uelewa wa umma kuhusu shughuli za bunge, una umuhimu mkubwa kwa kuwa bunge ni muhimili mkuu unaowakilisha sauti ya wananchi katika maamuzi ya kitaifa.

“Sababu kuu ya sisi kuja hapa ni kuwa tunataka kudhibiti wanafunzi kuja Nairobi kuja kujionea kinaechoendelea bungeni, watakapofika hapa watajionea kinachendelea kule, tunapanga kupeleka huduma zetu katika maonyesho mengine  katika kaunti nyingine, pia tunafanya hivi kupitia hafla nyengine kama kongamano la ugatuzi”, alisema Owino

Kwa upande wake Mwenyekiti wa maonyesho hayo Henry Nyagah, aliedokeza kuwa maonyesho ya mwaka huu yanaangazia kilimo biashara akisistiza umuhimu wa vijana kushiriki katika hafla hiyo inayoambatanishwa na matumizi ya teknolojia na mabadiliko ya tabia nchi.

Zaidi ya washirika 200 wanahudhuria maonyesho hayo ambayo pia yamevutia washirika saba kutoka mataifa ya nje.

Maonyesho hayo yanakamilika Jumapili Septemba 7, 2025.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version