Sports
Bingwa Wa Olimpiki Noah Lyles Kuanza Msimu Monaco
Bingwa wa Olimpiki mbio za mitaa 100 Noah Lyles wa Marekani kuanza rasmi msimu wake mjini Monaco Ufaransa katika msururu wa Diamond Ligi hii leo.
Mtimkaji huyo amekua na jeraha akiwa nje na sasa anarejea ulingoni akitarajiwa kuanza kutetea ubingwa wake katika mbio za mitaa 200 akitarajiwa kumenyana na bingwa wa Olimpiki mbio hizo Letsile Tebogo raia wa Botswana.
Lyles ndiye anashikilia rekodi bora katika mbio hizo baada ya kukimbia muda wa sekunde 19.46 mwezi wa April mwaka 2020 ila hajashiriki katika mashindano yoyote huu msimu.
Tebogo alirejea kwa kishindo wikendi iliopita na kushinda mbio za mitaa 200 mjini Eugene Oregon Marekani kwa muda wake bora wa sekunde 19.76 licha ya kuwa na msimu mbovu hadi sasa na amesema kwamba lengo lake ni kufanya kweli mjini Monaco Ufaransa.