Entertainment

Bilioni 7.1 kwa Ndoa, Harusi ya Bezos Yatikisa Dunia

Published

on

Mastaa wakubwa duniani wakiwemo Kim Kardashian, Bill Gates, na Oprah Winfrey wamewasili Venice, Italia, kwa ajili ya kuhudhuria harusi ya kifahari ya mwanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos, na mchumba wake Lauren Sanchez.

Wasanii wengine mashuhuri kama Usher, Kylie Jenner, na Ivanka Trump walionekana wakielekea eneo la tukio kwa kutumia boti za maji, kwa ajili ya hafla hiyo inayotarajiwa kugharimu zaidi ya euro milioni 40 (takriban Shilingi bilioni 7.1).

Licha ya maandamano yanayoendelea mjini humo kutoka kwa wanaharakati wanaopinga tukio hilo kwa mabango yaliyoandikwa “Hakuna Nafasi kwa Bezos”, maandalizi ya sherehe ya siku tatu yanaendelea bila kusitishwa.

/Photo Courtesy: Reuters

Taarifa zinaeleza kuwa wageni mashuhuri mamia wamethibitisha kuhudhuria, wakiwemo Kim Kardashian, Mick Jagger na Leonardo DiCaprio.

Lauren Sanchez, licha ya kutokuwa maarufu kama Bezos, ana historia ya kuvutia katika vyombo vya habari. Ana watoto watatu: mmoja kutoka kwa uhusiano na nyota wa NFL Tony Gonzalez, na wawili wengine kutoka ndoa yake ya zamani na wakala wa Hollywood, Patrick Whitesell.

Sanchez alikutana na Bezos kupitia kazi ya upigaji picha wa angani kupitia kampuni yake Black Ops Aviation, ambayo ilifanya kazi na Blue Origin ya Bezos.


Uhusiano wao ulianza kuzungumziwa mapema mwaka 2019, wakati huo Bezos alitangaza talaka na mkewe wa zamani MacKenzie Scott. Miezi michache baadaye, Sanchez naye aliwasilisha talaka kwa Whitesell.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version