Connect with us

Entertainment

Bilioni 7.1 kwa Ndoa, Harusi ya Bezos Yatikisa Dunia

Published

on

Mastaa wakubwa duniani wakiwemo Kim Kardashian, Bill Gates, na Oprah Winfrey wamewasili Venice, Italia, kwa ajili ya kuhudhuria harusi ya kifahari ya mwanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos, na mchumba wake Lauren Sanchez.

Wasanii wengine mashuhuri kama Usher, Kylie Jenner, na Ivanka Trump walionekana wakielekea eneo la tukio kwa kutumia boti za maji, kwa ajili ya hafla hiyo inayotarajiwa kugharimu zaidi ya euro milioni 40 (takriban Shilingi bilioni 7.1).

Licha ya maandamano yanayoendelea mjini humo kutoka kwa wanaharakati wanaopinga tukio hilo kwa mabango yaliyoandikwa “Hakuna Nafasi kwa Bezos”, maandalizi ya sherehe ya siku tatu yanaendelea bila kusitishwa.

/Photo Courtesy: Reuters

Taarifa zinaeleza kuwa wageni mashuhuri mamia wamethibitisha kuhudhuria, wakiwemo Kim Kardashian, Mick Jagger na Leonardo DiCaprio.

Lauren Sanchez, licha ya kutokuwa maarufu kama Bezos, ana historia ya kuvutia katika vyombo vya habari. Ana watoto watatu: mmoja kutoka kwa uhusiano na nyota wa NFL Tony Gonzalez, na wawili wengine kutoka ndoa yake ya zamani na wakala wa Hollywood, Patrick Whitesell.

Sanchez alikutana na Bezos kupitia kazi ya upigaji picha wa angani kupitia kampuni yake Black Ops Aviation, ambayo ilifanya kazi na Blue Origin ya Bezos.


Uhusiano wao ulianza kuzungumziwa mapema mwaka 2019, wakati huo Bezos alitangaza talaka na mkewe wa zamani MacKenzie Scott. Miezi michache baadaye, Sanchez naye aliwasilisha talaka kwa Whitesell.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Entertainment

Sijakataa Kuchangiwa, Ila Nipewe Heshima, Nyevu Fondo Afunguka

Published

on

Muunda maudhui maarufu Pwani, Nyevu Fondo, amefunguka sababu zake za kukataa pesa za mchango wa matibabu zilizochangishwa na Presenter Jakki.

Presenter Jakki, bila kumjulisha Nyevu, alianzisha kampeni ya mchango wa matibabu kwa jina lake baada ya kujua Nyevu anaugua, akiwahamasisha mashabiki na wafuasi wake kutuma msaada wa fedha akishiriki picha za Nyevu Fondo kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza hewani kwenye kipindi cha Janjaruka 254, Nyevu alisema wazi kuwa hana tatizo na watu kumchangia, lakini alikerwa na jinsi jambo hilo lilivyofanywa bila ushauriano:

“Mimi sijakataa kuchangiwa. Ni kitu poa. Kitu ambacho kinaniumiza ni kuwa kwa nini hakuniuliza mimi mwenyewe, naugua nini na nahitaji msaada aina  gani? Je, ule ugonjwa unahitaji msaada wa aina gani ama kile kitu nachougua kinahitaji msaada ama ala?”

Awali kwenye ukurasa wake wa Facebook Nyevu Fondo aliandika;

“Presenter Jacky, natumai uko salama dadangu. Kwanza, nashukuru kwa jitihada zako na za followers wako kunichangia – ni ishara ya upendo na utu. Lakini ujumbe wangu kwako ni huu: kabla ya kuchukua hatua kama hiyo tena, tafadhali niulize mimi binafsi kwanza. Wazo lako lilikuwa zuri upande wako, lakini kwangu halikukaa vizuri kwa sababu sikupewa nafasi kueleza hali yangu. Kwa sasa, sina uhitaji wa mchango huo kwani ninao msaada kutoka kwa Betty Kache Mwavuo, Hon. Oscar Wanje, na baadhi ya followers wanaonijali kama Mche Mtsumi na wengine wa Team Gulf.”

Hata hivyo Presenter Jakki hajanyamaza. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Jakki amejibu kwa hisia nzito, akieleza kusikitishwa na jinsi nia yake njema ilivyotafsiriwa vibaya mbele ya umma.

Hapa chini ni kauli yake kamili:

“Binadamu mbona tuna roho nyepesi kama korosho? 😢 Kwa nini mnanitengenezea taswira mbaya mbele ya hadhira yangu, ilhali nia yangu ilikuwa njema? Sitaki sifa wala umaarufu—nilitaka kusaidia kwa moyo wa huruma. Kumbukeni, kuna leo na kesho… na mitandao haitasahau kamwe. INTERNET NEVER FORGETS.”

“Kwa kuwa Nyevu Fondo hajaweza kupokea mchango huu, nimeamua pesa hizi nizielekeze kwenye kituo cha watoto yatima (Children’s Home) zikawe baraka kwa wengine. Labda Mungu ataniona na kunibariki. Kwa yote, nawaombea baraka – watu wa Mungu tuchukuliane kwa upendo.”

Awali Nyevu aliandika

Continue Reading

Entertainment

Penzi Lao Lazaa Matunda: Jux na Priscilla Watarajia Mwana

Published

on

Binti wa mwigizaji mashuhuri wa Nollywood, Iyabo Ojo, ambaye ni Priscilla Ojo, na mumewe, nyota wa muziki kutoka Tanzania Juma Jux, wametangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza.

Wapenzi hao walishiriki habari hizo njema kupitia mtandao wa Instagram kwa picha maridadi za ujauzito, ambapo Priscilla alionekana akionyesha tumbo lake la ujauzito. Picha hizo zilifuatana na maandishi mafupi: “Mum & Dad.”

Safari ya kimapenzi ya wawili hao imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu, ikijumuisha harusi kadhaa zilizofanyika nchini Nigeria na Tanzania, hatua ambayo iliangazia muunganiko wa tamaduni zao mbili.

Juma Jux alimvisha pete ya uchumba Priscilla mara mbili, ambapo ombi la pili lilikuwa la kipekee na lisilosahaulika, lililofanyika jijini Lagos, Nigeria.

Wapenzi hao waliadhimisha safari yao ya ndoa kwa sherehe mbalimbali, zikiwemo harusi ya kitamaduni ya Kiyoruba, harusi ya kanisani (white wedding), na sherehe nyingine zilizoandaliwa kwa fahari kubwa mnamo Aprili 17 na 19, zote zikiwa jijini Lagos.

Kadiri wanavyojiandaa kwa ujio wa mtoto wao wa kwanza, pongezi na salamu za heri kutoka kwa mashabiki na jamaa zimekuwa zikitiririka kwa wingi.

Continue Reading

Trending