Business
Biashara ya Matikiti Malindi Yadorora Msimu wa Mvua
Biashara ya kuuza matikiti maji mjini malindi kaunti ya kilifi imedorora msimu huu wa mvua ikilinganishwa na wakati wa kiangazi.
Kulingana na Edward Hinzano mchuuzi wa matunda hayo ni kuwa wakati wa kiangazi wateja walikuwa wengi hali ambayo iliwapelekea kupata faida zaidi ikilinganishwa na sasa.
Akiongea na meza yetu ya biashara Hinzano anasema kuwa wateja wamepungua na kusababisha hasara kwani matunda yanarabika.
Aidha amesema mvua ambayo inaendelea kunyesha pia inachangia kuharibika kwa matunda hayo kwani punde yakinyeshewa huharibika na kusababisha hasara zaidi.
“Msimu huu wa mvua biashara iko chini kwa sababu kuna baridi hivyo wateja wengi hawatumii hali ambayo inafanya biashara kuwa ngumu.”