Sports

Beldine Odemba Angali Kocha Wa Starlets.

Published

on

Mkufunzi wa Harambee Starlets Beldine Odemba atarejea kunoa tena kikosi hicho kwenye kinyanganyiro cha Cecafa ukanda wa Afrika Mashariki nchini Tanzania.

Haya yanajiri saa chache tu baada ya mwalimu huyo kubatilisha uwamuzi wake wa awali wa kujiuzulu wadhifa wake kwa kukosa ungwaji mkono kwenye majukumu yake ndaani ya vipusa hao.

Hata hivyo inaaminika baada ya kikao na Rais wa FKF Hussein Mohammed mwafaka imepatikana na sasa kocha huyo anasalia usukani kuiongoza Starlets kombe la cecafa taji ambalo linaanza mwishoni mwa jumaa.

Kocha huyo ambaye ni bingwa na kilabu ya Kenya Bullets alitangaza kujiuzulu baada ya kichapo cha magoli 5-1 mikononi mwa Morocco mechi ya kirafiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version