News

Baadhi ya wazee wa Kaya kaunti ya Kilifi wataka kuwe na kitengo cha wazee serikalini

Published

on

Mzee wa Kaya na pia mchungaji wa dini ya jadi maarufu Gohu, kwenye muungano wa kitamaduni wa MADCA kaunti ya Kilifi Edward Kazungu maarufu kama Kazungu wa Hawe Risa amesema  kunapaswa kuwa na kitengo cha wazee serikalini ambacho kitakuwa kinawashauri viongozi.

Akizungumza na Coco Fm, Hawe Risa amesema wazee wana busara na mchango mkubwa katika kutoa ushauri nasaha kwa viongozi ili watekeleze majukumu yao ipasavyo kwa manufaa ya wananchi.

Hawe Risa amesema viongozi wengi nchini wanashauriwa na wanasiasa hali ambayo inaendelea kusababisha kutokutekelezwa kwa miradi ya maendeleo kwani ushauri wanaotoa ni wa kisiasa na kwa manufaa yao binafsi.

Vilevile, Hawe Risa amesema kuna raslimali nyingi katika kaunti ya Kilifi na ikiwa Gavana wa kaunti hii ya Kilifi Gedion Maitha Mung’aro angekuwa na washauri wanaofaa, raslimali hizo zingetumika katika kuiboresha kaunti hii kimaendeleo.

Wakati huohuo Hawe Risa ametoa wito kwa serikali kuu kuimarisha huduma za matibabu kwa wazee kwani wanahangaika zaidi katika kutibiwa kwani wengi wao hawana fedha licha ya bima mpya ya matibabu ya SHA kuanzishwa nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version