Sports
Arsenal Kumpata Mshambulizi Gyokeres Bado Iko Kibarua
Matumaini ya Kilabu ya Arsenal kunasa huduma za mshambulizi wa Sporting Lisbon Victor Gyokeres huenda yakagonga mwamba.
Haya yanajiri baada ya kizingiti cha kipenge cha uhamisho wa mchezaji huyo kugura Lisbon kutoafikiwa mpaka sasa na hivyo uhamisho huo uko katika njia panda hadi sasa kulingana na jarida la Dail Mail barani Ulaya.
The Gunners walikua tayari wamekubaliana na matakwa ya Gyokeres kimkataba huku Lisbon ikidai pauni milioni 67 ila mambo bado hayajatatuliwa kutokana na kipenge chake cha uhamisho aliondikisha na Sporting Lisbon alipojiunga nao.