News
Aliyekuwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari Afariki Mjini London
Aliyekuwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amefariki katika Hospitali Moja Mjini London leo Jumapili Julai 13, akiwa na umri 82.
Kiongozi huyo ambaye aliitawala Nigeria kwa vipindi viwili kidemokrasia, aliingia madarakani kwa mara ya kwanza kupitia mapunduzi ya mwaka1983, kabla ya kupinduliwa tena miaka miwili bàadaye.
Kisha mnamo mwaka 2015 akaandikisha historia kwa kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kumshinda Rais aliye mamlakani na kuchukua hatamu ya kuliongoza Taifa la Nigeria.
Buhari alichaguliwakwa kwa kipindi Cha pili cha miaka minne mnamo 2019 kabla ya kustaafu.
Rais wa sasa nchini humo Bola Ahmed Tinubu ametuma risala za rambi rambi kwa Mke wa Buhari na familia yake, huku akimtuma Naibu wake kusafiri hadi mjini London kuufanya matayarisho ya kusafirishwa kwa mwa mwili wa Marehemu Buhari hadi nchini Nigeria.
Buhari ambaye anatokea jamii ya Fulani, alizaliwa katika Jimbo la Daura Katsina, Kaskazini mwa Nigeria mnamo 1942 na kisha bàadaye kujiunga na mafunzi ya kijeshi katika jimbo la Kaduna.
Alianza kupata umaarufu wale wa kisiasa mnamo mwaka 1975 kufuatia mapinduzi ya Rais wa nchi hiyo wakati huo Yakubu Gowon.
Baadaye alichaguliwa kuwa Gavana wa kijeshi wa Jimbo la Borno ambalo katika miaka ya hivi majuzi limekumbwa na mashambulio makali kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Boko Haram.