Sports
Rashford Kujiunga na Barcelona Kuimarisha Safu ya Ushambuliaji
Mchezaji nyota wa Manchester United, Marcus Rashford, sasa yupo sokoni na anapatikana kwa vilabu vyote kwa ada ya uhamisho ya takriban pauni milioni 40.
Tetesi zinasema kwamba, klabu ya Barcelona bado inaendelea kumfuatilia mshambuliaji huyo, ikiwa ni mwendelezo wa nia waliyoonyesha tangu mwezi Januari mwaka huu.
Hapo awali, dili hilo halikukamilika kutokana na kutokuwepo kwa uuzwaji wa mchezaji mwingine ambaye angewezesha uhamisho huo.
Hivi karibuni, mwandishi wa soka Toni Juanmartí (@tjuanmarti) ameripoti kuwa wawakilishi wa Rashford wamekutana tena na viongozi wa Barcelona kwa mazungumzo zaidi kuhusu uwezekano wa uhamisho huo.
Rashford ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanne waliopo kwenye orodha ya Barcelona, wanaochunguzwa kwa ajili ya kuimarisha kikosi hicho msimu ujao.
Ingawa bado hakuna uthibitisho rasmi kuhusu mafanikio ya mazungumzo hayo, uwezekano wa Rashford kujiunga na Barcelona bado upo wazi.