Sports

Mujinga Kutoshiriki Mashindano ya Kipkeino Classic

Published

on

Mwanariadha nyota kutoka Uswisi, Mujinga Kambundji, hatashiriki katika mashindano ya Kipkeino Classic yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi, Mei 31 katika uwanja wa michezo wa Ulinzi, jijini Nairobi.

Kupitia ujumbe alioweka kwenye ukurasa wake wa Instagram Ijumaa iliyopita, Kambundji amethibitisha kuwa hatashiriki tena katika mashindano ya msimu huu wa riadha. Ameeleza kuwa sababu ya kusitisha msimu wake ni ujauzito, na ameahidi kurejea tena uwanjani mwaka ujao.

Kwenye taarifa yake Mujinga alisema, “Msimu umeisha, kwa sababu nzuri zaidi. Nina furaha sana kuwajulisha kuwa muujiza wetu mdogo uko njiani.” Kauli hiyo iliambatana na picha yake akionyesha matokeo ya uchunguzi wa ultrasound, ambao hutumika kuangazia maendeleo ya fetusi na tathmini ya ujauzito.

Kambundji, mwenye umri wa miaka 32, ni mshindi wa medali za dunia mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na medali ya shaba katika mashindano ya dunia ya riadha pamoja na mafanikio kwenye mashindano ya ndani ya baridi. Ametangaza kuwa anatarajia kurejea tena kwenye mashindano mwaka wa 2026.

Awali, mashindano ya Kipkeino Classic yalipangwa kufanyika katika uwanja wa Nyayo, lakini kutokana na ukarabati unaoendelea, yamehamishiwa katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version