News
Papa Leo XIV Achangulia Rasmi
Kadinali Robert Francis Prevost kutoka taifa la Marekani ndiye Papa mpya aliyechaguliwa kuongoza Kanisa Katoliki kote duniani.
Kadinali Prevost amechagua jina la Papa Leo XIV.
Papa Leo XIV ana umri wa miaka 69 na alizaliwa Septemba 14 mwaka wa 1955 na ana uraia wa taifa la Peru na Marekani.
Hatua hiyo, ameafikiwa baada ya Makadinali kutekeleza jukumu lao la kitume la kupigia kura Kiongozi ambaye atachukua jukumu la kuongoza Kanisa Katoliki kote duniani.
Makadinali 133 walikuwa wakiendeleza mchakato wa kumchagua Papa mpya katika kipindi cha siku mbili katika Kanisa la Sistine mjini Vatican na hatimaye kuafikia kumpata Papa Leo XIV ambaye ataongoza waumini wa Kanisa Katoliki.
Papa Leo XIV, anatarajiwa kuhakikisha anaendeleza mshikamano wa waumini na amani kote ulimwenguni ikiwemo kutafuta mwafaka wa mizozo ya vita katika mataifa mbalimbali.
Papa Leo XIV atakuwa Papa wa 267.