News
Waziri Murkomen kutathmni hali ya usalama kwenye kaunti za Meru, Embu na Tharaka Nithi
Waziri wa Usalama wa ndani Kipchumba Murkomen, anazuru kaunti za Meru, Tharaka Nithi, na Embu, kutathmini hali ya usalama.

Waziri Kipchumba Murkomen akiwa kaunti ya Meru/picha kwa hisani
Murkomen ambaye kwa sasa y uko kwenye kaunti ya Meru, atashiriki mkutano na kamati ya usalama ya Meru, kabla ya kuzuru kituo cha usajili wa vitambulisho na kampeni dhidi ya mihadarati inayoongozwa na mamlaka ya kukabiliana na pombe na dawa za kulevya (NACADA).
Aidha, Murkomen atashiriki misururu ya mikutano na wananchi katika uwanja wa michezo wa Kinoru kuhusu maswala ya usalama.
Mikutano ya Jukwaa la Usalama uhudhuriwa na maafisa wa serikali ya taifa kuanzia kwa kamishna wa kaunti hadi kwa naibu wa chifu, viongozi wa jamii, wafanyabiashara na vijana.
Katika kaunti ya Meru, Murkomen ataangazia upya swala la wizi wa mifugo katika mpaka wa Meru na Isiolo.
Kaunti ya Meru pia inakabiliwa na mizozo ya muda mrefu ya ardhi, hususan katika mpaka wa Meru na Tharaka Nithi.