News

Wawakilishi Wadi kaunti ya Kilifi Wazibana Makonde

Published

on

Kizaazaa kilishuhudiwa katika majengo ya bunge la kaunti ya Kilifi baada ya Wawakilishi wadi ambao ni Wanachama wa Kamati ya bajeti katika bunge hilo kutofautiana kuhusu uongozi na uawajibikaji.

Hali hiyo ilisababisha Mwakilishi wadi maalum Elina Mapenzi kuzabwa makonde na Wawakilishi wadi wawili wa kiume akiwemo Mwakilishi wadi ya Shella Twahir Abdulkarim na Mwakilishi wadi ya Watamu Ibrahim Matumbo ambao wanaegemea upande wa Gavana wa Kilifi Gedion Mung’aro wakati wa kikao cha kutathmini masuala tata kuhusu bajeti ya mwaka wa kifedha 2025/26.

Kulingana na baadhi ya Wawakilishi wadi waliokuwa katika kikao hicho, kizaazaa hicho kilisababisha Mwakilishi wadi huyo maalum kupata majeraha wakati wa vurugu hizo kwenye kikao hicho cha kamati ya bajeti.

Kizaazaa hicho pia kilichangiwa zaidi pale wanachama wa kamati hiyo walipochukizwa na hatua ya Spika wa bunge hilo Teddy Mwambire kuagiza bunge kujadili mchakato wa bajeti ya mwaka huu bungeni na wala sio kamati hiyo ya bajeti kwa kuambatana na sheria.

Wawakilishi wadi hao, sasa wanadai kwamba watawasilisha hoja bungeni ya kutokuwa na Imani na Spika Mwambire ili kumtimua uongozini kwa kukiuka kanuni za bunge hilo.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Shirika la Kilifi Mum’s Kibibi Ali amekashfu vikali kitengo hicho, akikitaja kama unyanyasaji wa kijinsia kwa viongozi wa kike katika kaunti hiyo.

0 Comments

  1. Nasser Mohammed

    May 14, 2025 at 11:33 am

    Kuna barua nimemuandikia spika kama mwananchi mzalendo,naomba ni share na nyinyi tafadhali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version