News

Wanaharakati wamepinga mchakato wa mazungumzo ya kitaifa

Published

on

Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kaunti ya Mombasa yamepinga mchakato wa mazungumzo ya kitaifa yakisema matatizo yanayowakumba wakenya tayari yanajulikana.

Wanaharakati hao wakiongozwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la Vocal Afrika, Hussein Khalid walidai serikali ya Kenya Kwanza imeshindwa kutekeleza matakwa ya vijana wa kizazi cha Gen z licha ya ahadi tele baada ya maandamano ya mwezi Juni mwaka 2024 ikiwemo fidia kwa walioafariki katika maandamano hayo, kukabiliana na ufisadi pamoja na maafisa waliohusika wakabiliwe kisheria.

Wanaharakati hao pia walidai mazungumzo hayo ni njama ya kufumbia jicho matukio ya ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini.

“Raila Amolo Odinga tekeleza makubaliano na serikali kuu. Na ikiwa utafanya hivyo hakuna haja ya mazungumzo ama chochote kile’’, alisema Khalid.

Vilevile, Wanaharaki hao walisema ikiwa serikali kuu iko na ushahidi iwakamate waliohusika na iwafungulie mashtaka kwa mujibu wa sheria.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version