National News
Wakulima wa Taveta Walalamikia Uharibifu wa Mimea Yao
Wakaazi wa Mariwenyi gatuzi dogo la Mwatate kaunti ya Taita Taveta wamelalamikia uharibifu mimea yao unaosababishwa na wanyamapori katika eneo hilo.
Kisa cha hivi karibuni ni kuharibiwa kwa ekari 5 za shamba la mihogo ambao wanasema uharibifu huo umesababishwa na Ndovu hata mashamba yao huku wakiripoti kwamba mimea kama vile migomba na matikiti maji imeharibiwa na ndovu pasipo na fidia.
Wamelilaumu Shirika la huduma kwa wanyamapori, KWS kwa kile walichosema kuwa limezembea katika kuwadhibiti wanyamapori hao wanaoendelea kuwasababishia hasara.
Aidha wanaitaka serikali kupitia Shirika la KWS kuingilia kati swala hilo, wakisema wanapitia ugumu kwani tegemeo lao ni Kilimo ila mimea yao imekuwa ikiharibiwa na wanyamapori.
Wameeleza kusikitishwa na Shirika la KWS, wakisema kwamba Shirika hilo inawajali sana wanyamapori kuliko binadamu kwani limekosa kuangazia masaibu yanayowakumba mashinani.