News

Wakristu Waadhimisha Siku ya Ijumaa Kuu

Published

on

Waumini wa Kanisa Katoliki kote ulimwenguni wamejitokeza kuadhimisha ibada ya njia ya msalaba, wakiashiria ukumbusho wa mateso ambayo Yesu Kristu alipitia kabla ya kufa na kufufuka kulingana na imani ya dini hiyo.

Ibada ya njia ya Msalaba, huadhimishwa kila mwaka baada ya waumuni wa Kanisa Katoliki kukamilisha kipindi cha kufunga na kusali ambayo hutambulika kama Kwaresma, kisha Jumapili ya Matawi na hatimaye kipindi cha Pasaka ambayo huanza rasmi na siku ya Ijumaa Kuu.

Kulingana na Kanisa Katoliki, siku ya Ijumaa kuu, ni kipindi cha mwisho cha maisha ya Yesu Kristu kabla ya kuteswa, kufa na hatimaye kufufuka siku ya tatu ambapo waumuni hao kuadhimisha sherehe za sikukuu ya Pasaka.

Viongozi mbalimbali wa kidini katika Kanisa Katoliki la St Patrick Parokia ya Kilifi wakiongozwa na Padre Marsellous Okello, wamehimiza umuhimu wa unyenyekevu na amani jinsi Yesu Kristu alivyoyaweka maisha yake kwa Mungu.

Hata hivyo maafisa wa usalama wameahidi kuimarishwa kwa usalama katika maeneo mbalimbali ya Pwani ikiwemo maeneo ya burudani, fuo za bahari hindi pamoja na vituo vya kuabiri magari ya uchukuzi wa umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version