County
Wakereketwa wa Siasa Magarini Walitaka Jopo la Uteuzi wa Makamishna Wapya wa IEBC Kukamilisha zoezi kwa Muda Unaofaa
Wakereketwa wa maswala ya kisiasa katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wamelitaka jopokazi la uteuzi wa Makamishna wapya wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kukamilisha kwa muda unaofaa uteuzi wa Makamishna hao.
Wakiongozwa na Emmanuel Ngumbao, wakereketwa hao wamesema hatua hiyo itasaidia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Magarini kwani eneo bunge hilo limesalia bila ya mwakilishi bungeni.
Ngumbao amehoji kwamba eneo bunge hilo limekosa maendeleo kwa mda mrefu kutokana na Mahakama kuu kubatilisha uchaguzi wa Harrison Kombe aliyekuwa mbunge wa eneo hilo.
Wakati huo huo amesisitiza haja ya swala la uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Magarini kupewa kipaumbele baada ya kuapishwa kwa Makamishna wapya wa IEBC.