News
Wakaazi Waonywa Dhidi ya Kuranda Onyo Katika Fuo za Bahari Hindi
Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Reginald Omaria amewaonya wakaazi dhidi ya kuranda randa ovyo katika fuo za bahari hindi katika masaa yasiokubalika na kwamba atakayepatikana atakabiliwa kisheria.
Omaria anasema kama njia mojawapo ya kuimarisha usalama hakuna mgeni ama mwenyeji anayeruhusiwa kuwa ufuoni baada ya saa kumi na mbili jioni msimu huu wa sherehe ya pasaka.
Kiongozi huyo wa usalama amewataka wazazi kuwalinda watoto wao ili kuwaepusha na visa vya uvunjaji wa sheria.
Kwa upande wake Kamishna wa kaunti ya Kwale Stephen Orinde amesema oparesheni zaidi za kiusalama zinaendelea katika kaunti hiyo.