County
Wakaazi wa Msabaha Wanaitaka Kaunti Kuikarabati Barabara ya Mbarakachembe
Wakaazi wa maeneo ya Mashamba na Msabaha wadi ya Ganda katika kaunti ya Kilifi wanaitaka serikali ya kaunti kupitia idara ya barabara kuifanyia ukarabati barabara ya Imani Childrens Home kuelekea Mbarakachembe.
Wakiongozwa na Daniel Mwachima, wakaazi hao wameitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kuweka mikakati ya kupunguza mchanga ulio katika barabara hiyo unaotatiza shughuli za uchukuzi.
Mwachima amesema barabara hiyo iko katika hali mbaya na huenda itachangia ajali iwapo haitashuhulikiwa kwa haraka.
Kauli yake imeungwa mkono na mzee wa kijiji cha Msabaha, Mwakudza Katana ambaye amesisitiza haja ya barabara hiyo kuwekwa Moramu ili kupunguza visa vya ajali.