National News

Wakaazi wa Diani Wanaitaka DCI Kufanya Upekuzi wa Maduka ya Kuuza Dawa

Published

on

Wakaazi wa Diani eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale wanaitaka idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI kufanya upekuzi wa maduka ya kuuza dawa.

Wakaazi hao wanadai kwamba huenda maduka ya kuuza dawa yanachangia ongezeko la visa vya utovu wa usalama.

Wakiongozwa na Rehema Shee, wakaazi hao wamesema baadhi ya vijana hununua dawa kutoka kwa maduka hayo kinyume na sheria, wakisema kuna haja ya idara ya usalama kwa ushirikiano na maafisa wa bodi ya dawa na sumu nchini kufanya msako wa maduka hayo.

Aidha wamesema dawa hizo kuathiri akili za vijana hao na kuchangia madhara makubwa katika jamii.

Kwa upande wao mkuu wa Idara ya DCI kaunti ya Kwale Juliana Muthini imewahakikishia wakaazi kwamba wataanzisha oparesheni ya kukagua maduka hayo.

Muthini amesema tayari wameweka mikakati ya kuanzisha kituo cha kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo ya Diani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version