News
Wakaazi Kwale waonywa dhidi ya upepo mkali baharini
Wakaazi na wavuvi wanaotumia ufuo wa bahari hindi katika eneo la Diani kaunti ya Kwale wameonywa kuwa waangalifu zaidi dhidi ya upepo mkali unaoshuhudiwa baharini.
Kulingana na afisa wa idara ya hali ya anga katika kaunti ya Kwale Danson Ireri, iwapo wakaazi na wavuvi watajitenga kuzuru katika fuo za habari hindi wakati huo ambapo kuna upepo mkali basi watajiepusha na majanga.
Ireri alisema upepo huo unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kati ya kilomita 13 hadi 20 kwa saa.
Afisa huyo aliongeza kuwa Kwale inatarajiwa kuwa na baridi na mawingu mazito huku maeneo machache yakipokea manyunyu ya mvua.
Viwango vya joto vinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 18 hadi 32.
Taarifa ya Mwanahabari wetu.