Business
Wafanyabiashara Mombasa: Vurugu Zadidimiza Biashara na Uchumi
Wafanyibiashara kaunti ya Mombasa wamesema kuwa vurugu ambazo zimekuwa zikishuhudiwa mara kwa mara humu nchini zimesababisha kudorora kwa biashara nyingi humu nchini.
Wakiongozwa na Simoni Owa wafanyibiashara hao walisema kuwa waekezaji wengi wamehamia mataifa jirani wakihofia biashara zao kuharibiwa hali ambayo imeathiri uchumi.
Kulingana na Owa hali mbaya ya kiuchumi, kupanda kwa gharama ya ushuru, imepelekea waekezaji wengi pia kuhamia mataifa jirani, jambo ambalo pia limesababisha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.
Aidha waliitaka serikali kuu kuweka mikakati ya kuhakikisha vurugu hizo zinasitishwa ili kutetea uchumi wa taifa.