Sports

United Yaweka Ofa Ya Pili Kupata Mbeumo

Published

on

Kilabu ya Manchester United kimewasilisha ofa ya pili ya pauni milioni 60 kwa kiungo mshambulizi wa Brenford Bryan Mbeumo raia wa taifa la Cameroon.

Haya yanajiri wiki mbili tu baada ya ofa ya kwanza ya Pauni millioni 55 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kukataliwa na Brenford.

Mvamizi huyo alikua nguzo muhimu kwa The Bees akifunga magoli 20 na kuchangia 9 msimu uliokamilika huku kilabu hiyo ikimaliza ndaani ya kumi bora.

Vilabu vingi vimekua vikimmezea mate ikiwemo,Arsenal na  Tottenham Hotspurs pia wakiwinda huduma zake,hata hivyo Mbeumo amesema chaguo lake ni Mancheter United.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version