Utafiti uliyofanmywa na kampuni ya utafiti ya Infotrak umeonyesha wazi kwamba asilimia 57 ya wakenya wanasema kwamba taifa linaelekea mahali pabaya, asilimia 17 wakiridhishwa na mwelekeo wa taifa huku asilimia 21 wakikosa kuweka wazi mtizamo wao.
Utafiti huo pia uliweka wazi kwamba wakenya wengi wanalalamikia gharama ya juu ya maisha na ukosefu wa ajira ambao umesababishwa na utawala mbaya.
Akitoa ripoti ya utafiti huo, Meneja wa Utafiti kutoka Infotrak Johvine Wanyingo alisema asilimia 66 ya wakenya wanaamini kwamba gharama ya juu ya maisha imechangia pakubwa hayo hiyo.
Wanyingo alisema utafiti huo ambao ulifanywa mwezi Agosti mwaka huu na kuhusisha wakenya 2,400 kote nchini umeonyesha wazi kwamba asilimia 30 ya wakenya wakilalamikia ukosefu wa ajira, asilimia 15 wakilalamikia utawala mbaya na asilimia 15 wakikosa bima ya SHA.
“Mwezi Septemba mwaka jana angalia asilimia ilikuwa nusu kwa nusu lakini sasa wakenya umeonyesha kuchoka na hali ngumu ya maisha inayoendelea nchini”, alisema Wanyingo.
Hata hivyo baadhi ya wakenya waliohojiwa walikuwa na mtizamo tofauti kwani asilimia 41 wamesema taifa limeshuhudia amani na utulivu, asilimia 37 wakisema serikali imetekeleza maendeleo na asilimia 28 wakisema uchumi wa nchi unaimarika.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
