COCO fm yang’aa kwenye tuzo za Africa Champions Awards 2025

COCO fm yang’aa kwenye tuzo za Africa Champions Awards 2025

Kituo cha redio cha COCO FM kimeng’aa katika tuzo za kila mwaka makala ya saba za Africa Champions Awards zilizoandaliwa jijini Mombasa.

Katika tamasha ya tuzo hizo Coco Fm imetambuliwa kama kituo bora na kinachokua kwa kasi zaidi nchini Kenya.

Vile vile Coco FM imetwaa tuzo ya kituo bora kinachopeperusha matangazo yake kupitia sauti na video, zinazopeperushwa hewani kupitia redio na mitandao ya kijamii.

Tuzo nyengine imemwendea mwanahabari nguli Lolani Kalu kutokana na taarifa na makala anazoandaa hasa zinazoangazia maisha ya mwananchi wa kawaidia.

Akizungumza katika hafla hiyo, msimamizi wa kituo hicho Said Kashindo alipongeza juhudi za watangazaji wa COCO FM kwa kuangazia taarifa sahihi na zinazohusu maisha ya wakaazi vile vile matangazo na vipindi bora.

Kashindo pia alimshukuru msikilizaji kwa kuamini matangazo ya stesheni ya Coco fm na kuahidi kuendelea kuwajuza mengi zaidi yanayofanyika nchini na hata ulimwenguni kwa ujumla.

Taarifa ya Joseph Jira.