Mahakama ya Kilifi katika kaunti ya Kilifi inatarajiwa kutoa uamuzi wa dhamana kwa mshukiwa wa wizi wa kimabavu Joel Kalume Robert maarufu Kalume Diga.
Hakimu wa Mahakama hiyo James Mwaniki aliagiza mshukiwa Diga kuendelea kuzuiliwa rumande hadi Disemba 21 mwaka wa 2025, ambapo Mahakama itatoa uamuzi iwapo mshukiwa anafaa kuachiliwa kwa dhamana au la.
Agizo hilo lilitolewa baada ya Kiongozi wa mashtaka Winnie Otieno kueleza Mahakama kwamba kulingana na ripoti ya afisa wa jamii, Diga hastahili kuachiliwa kwa dhamana kwani wanakijiji wanahamaki na huenda akauwawa.
Akijitetea mbele ya Hakimu Mwaniki, Diga alisema ana familia na watoto wanaomtegemea hivyo anaomba Mahakama hiyo kumwachilia kwa dhamana.
Ombi la Diga mbele ya Mahakama ni baada ya kukanusha mashtaka dhidi yake kwamba alitekeleza wizi wa mabavu wa pikipiki mjini Kilifi.
Taarifa ya Teclar Yeri.
