Sports
Stars Yapanda Msimamo Wa FIFA
Timu ya Taifa ya soka Harambee Stars imepanda nafasi mbili juu katika msimamo wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA kutoka 111 hadi 109 msimamo unaotolewa kila mwezi ukiwa ni msimamo wa mwezi jana.
Stars katika kipindi hicho ilicheza mechi mbili za kirafiki wakitoka sare na badaye wakishinda taifa la Chad magoli 2-1 ,Taifa la Uganda lingali la kwanza Afrika Mashariki wakiwa nafasi ya 97.
Taifa la Morocco linashikilia nafasi ya kwanza Barani Afrika na ni ya 12 ulimwenguni wakifutwa na mataifa ya Senegal kisha Misri katika nafasi ya pili na tatu.
Mabingwa wa Dunia Argentina ni ya kwanza kote ulimwenguni likifutwa na Uhispania,Ufaransa na Uingereza,nafasi ya pili tatu na nne mtawalia.