Sports

Sinner Bingwa Tennis Msururu Wa Wimbledon

Published

on

Mchezaji wa Tenisi anayeorodheshwa wa kwanza Ulimwenguni Jennik Sinner raia wa Italia amesema kwamba lengo lake ni kutawala dunia sasa baada ya kumpiku mwenzake Carlos Alcaraz na ksuhinda fainali ya taji la Wimbledon likiwa ni taji lake la kwanza.

Sinner alimpiku Alcaraz raia wa Uhispania kwa seti za 4-6, 6-4, 6-4, 6-4 na kuvunjilia mbali rekodi ya mhispania huyo ya kushinda taji hilo mara tatu mfululizo.

Mchezaji huyo amesema kwamba analenga kujiboresha hata zaidi akiwaonya wapinzani angali kutoa makali yake yote.

“Niko na umri wa miaka 23 na kwa sasa ningali kuwa katika ubora wangu narudi kujipanga zaidi kwa ajili ya misururu mingine ila niko na imani ya kufanya kweli katika misuru ya Tenisi.”

Mchezaji huyo amfika katika fainali nne na kushinda tatu za Grandslam na amesema hataki kutoka hapo juu kuwa mchezaji bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version