News
Seneta Madzayo, anataka miili ya Shakahola Malindi kuzikwa kwa pamoja
Seneta wa kaunti ya Kilifi, Stewart Madzayo amegadhabishwa na kile alichokiita utepetevu katika serikali kuu kufuatia malimbikizi ya miili inayofukuliwa Shakahola inayohifadhiwa kwenye makafani ya hospitali ya Malindi kaunti ya Kilifi.
Katika mahojiano ya kipekee na Coco Fm, Madzayo alisema amewasilisha miswada kadhaa katika bunge la seneti kuhakikisha kwamba miili hiyo inashughulikiwa ila serikali kuu haijalibeba kwa uzito kwa suala hilo.
Madzayo alisema kuwa miili hiyo inazidi kujazana kwenye hifadhi ya maiti ya hospitali hiyo ya Malindi hali inayotatiza huduma za kuhifadhi miili ya wakaazi wa eneo hilo.
“Mochari imejaa miili ya Shakahola na miili hiyo sio ya watu wetu wa Kilifi maana ingekuwa ya watu wetu wangekuwa wamekwisha ichukua, sasa watu wetu wanakosa nafasi ya kuhifadhi miili ya wapendwa wao kwa sababau mochari imejaa” aliongeza Madzayo.

Baadhi ya miili iliyofukuliwa Shakahola na sasa inahifadhiwa katika makafani ya hospitali ya Malindi
Kufuatia hilo, Seneta Madzayo alitishia kuwa watachukua sheria mkononi kwa kuiondoa miili hiyo kwenye makafani sawa na kuzuia miili mingine kuwekwa kwenye hifadhi hiyo hadi pale utata huo utakapotatuliwa.
Taarifa ya Hamis Kombe