Sports

Real Madrid Kuanza Rasmi msimu Mpya wa Laliga Chini Ya Xabi Alonso

Published

on

Kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso, amesema maandalizi mafupi ya kabla ya msimu hayatakuwa kisingizio huku kikosi chake kikijiandaa kuanza kampeni ya La Liga nyumbani dhidi ya Osasuna leo usiku.

Mchezaji huyo wa zamani wa Real atakuwa akisimamia mchezo wake wa kwanza katika uwanja wa Santiago Bernabeu baada ya kuanza rasmi enzi yake kwenye Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani, ambapo Madrid walitinga hatua ya nusu fainali.

Awali ombi la Madrid la kuahirisha mechi yao ya ufunguzi wa ligi hadi tarehe nyingine lilikataliwa na viongozi wa soka la Uhispania, na kikosi hicho kimecheza mechi moja tu ya kirafiki tangu waliposhindwa 4-0 dhidi ya Paris Saint-Germain huko New Jersey mnamo Julai 9.

Alonso sasa anategemea usajili kadhaa wapya, akiwemo beki wa zamani wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, wakati Madrid wakilenga kufuta kumbukumbu ya mwisho mbaya wa enzi ya Carlo Ancelotti.

Madrid walitwaa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya na La Liga msimu wa 2023-24, lakini wakamaliza ligi ya ndani wakiwa wa pili nyuma ya mahasimu wao wakubwa Barcelona msimu uliopita, na wakaondolewa na Arsenal katika robo fainali ya Ulaya.

Alonso, ambaye aliiongoza Bayer Leverkusen kutwaa ubingwa wa Bundesliga na Kombe la Ujerumani miaka miwili iliyopita, amesema kwa tahadhari kuhusu matarajio yake jijini Madrid.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version