News

Rais Ruto atia saini mswada wa fedha wa 2025 kuwa sheria.

Published

on

Rais William Ruto ameidhinisha Mswada wa Fedha wa 2025.

Ruto alitia saini mswada huo kuwa sheria asubuhi ya alhamisi tarehe 26 juni 2025 katika ikulu ya Nairobi baada ya wabunge kupitisha sheria iliyopendekezwa wiki jana.

Ingawa mswada huo uliepuka kuwasilisha ushuru mpya kufuatia maandamano mabaya ya mwaka jana dhidi ya mswada wa fedha wa 2024/2025, baadhi ya vifungu vilikuwa na utata kama vile pendekezo la kutaka kuipa Mamlaka ya kitaifa ya ukusanyaji ushuru KRA uwezo wa kufikia data ya kibinafsi na ya kifedha ya walipa kodi.

Wabunge hatimaye waliuangusha walipokuwa wakiupigia kura kabla ya kutumwa kwa rais Ruto ili kuidhinishwa.

Waziri wa hazina ya kitaifa John Mbadi aliwasilisha bajeti ya shilinghi trilioni 4.2 katika mwaka wa kifedha wa 2025/26 bungeni mapema mwezi huu, na wizara yake inatarajia kukusanya hadi shilingi bilioni 30 katika mapato ya ziada kutoka kwa mswada wa huo wa fedha.

Wakati huo huo, rais Ruto pia alitia saini mswada wa uidhinishaji wa mwaka 2025, utakaoruhusu hazina ya kitaifa kuchukua shilingi trilioni 1.88 kutoka kwa hazina ya pamoja kwa mwaka wa kifedha wa 2025/26.

Mswada huo unaruhusu wizara, idara na mashirika kutumia shilingi bilioni 672 katika ugavi wa msaada, kama ilivyoidhinishwa na bunge.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version