News

Rais Ruto atangaza Agosti 27, kuwa Katiba Dei.

Published

on

Rais William Ruto ametangaza kwamba Agosti 27, itakuwa siku ya kitaifa ya Katiba Dei ambayo itakuwa ikiadhimishwa kila mwaka.

Tangazo hilo ambalo lilichapishwa katika gazeti rasmi la serikali linalenga kuadhimisha miaka 15 tangu taifa lipate Katiba mpya mwaka wa 2010 na kwamba itakuwa siku ya hamasisho kwa umma kuhusu vipengele vya Katiba.

Tangazo hilo la rais lilifafanua zaidi kwamba siku hiyo itakuwa siku ya kawaida ya kazi na wala sio siku ya kitaifa ya mapumziko na kwamba itawawezesha wakenya kufahamu masuala mbalimbali ya Katiba, utawala wa sheria na mazungumzo ya kitaifa.

Aidha lengo kuu la Katiba Dei ni kuangazia safari ya kidemokrasia ya Kenya na kuhimiza haki ya umma katika mijadala mbalimbali ya utawala kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kote nchini.

Hata hivyo himizo zaidi ni kwa mihimili tatu ya serikali, ngazi zote mbili za kiutawala na taasisi za kielimu zitahitajika kuandaa na kushiriki katika shughuli za umma ili kukuza uelewa wa Katiba na ushirikishwaji wa umma.


Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version