Sports
Rais Awahidi Basi Mpya Mabingwa Wa Ligi Kuu Police
Rais William Samoei Ruto ameahidi kununulia basi jipya Mabingwa wapya wa ligi kuu FKF PL Kenya Police kwa kazi kuntu waliofanya msimu huu.
Rais alitoa ahadi hiyo wakati wa kikao cha chakula cha asubuhi baada ya mwaliko ikuluni mapema leo ambapo aliweza kupongeza timu hiyo akiahidi pia atatembea nao msimu ujao katika juhudi zao za kueteta ligi hiyo ya taifa.
“Kama wachezaji na wanaspoti nichukua fursa hii kuwahukuru kwa kazi nzuri tutazidi kuwashika mkono nimeambiwa mnahitaji basi nzuri ,Nitawatafutia Basi nzuri kwa majukumu ya usafiri.”
Kwa upande wake Waziri wa Michezo Salim Mvurya amefichua kwamba hivi karibuni Wizara yake litazindua taji la Rais marufu kama Presidents Cup ambalo litaanza mashinani hadi kwneye taifa na kuanzishwa na rais mwenyewe.