Sports
Palmer apewa jezi namba 10 Chelsea
Kilabu ya Chelsea imetangaza kumpa jezi namba 10 kiungo mbunifu wa kilabu hiyo Cole Palmer raia wa Uingereza baada ya kuonyesha ubora wake tangu kusajiliwa kutoka kilabu ya Manchester City misimu miwili iliopita.
Jezi hilo limekua likivaliwa na mshambulizi wa taifa la Ukraine Mikhael Mudrykambaye amefungiwa kucheza kutokana na tuhuma za utumizi wa dawa za kulevya ama ulaji muuku jambo ambalo huenda limesababisha hatua hiyo kuchukuliwa na uongozi wa The Blues.
Timu Hiyo hata hivyo haijatoa ripoti yoyote kuhusiana na hatima ya mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 89 akitokea Shaktar Donesk ya Ukraine.
Mudryk mwenye umri wa miaka 24 alijiunga na Chelsea mwaka 2023 akifanikiwa kufunga magoli 5 katika mechi 53 ambazo ameshirikisha na kocha Enzo Maresca na hajachezea kilabu hiyo tangu mwaka jana akizidi kuwa gizani kwenye kilabu ya chelsea.