Sports
Osaka Na Azarenka Wafuzu Raundi Ya Pili Kabla ya Wimbledon
Wachezaji wa Tenesi kwa akina dada Naomi Osaka wa Japan na Victoria Azarenka wote wameweza kujikatia tiketi ya Raundi ijayo msururu wa Wimbledon baada ya kushinda mechi zao katika mechi za maandalizi Bad Homburg.
Osaka ambaye alikua anaorodheshwa wa kwanza wakati mmoja alimzidi mwenzake Olga Danilovic wa taifa la Serbia kwa seti za 7-6 (8/6), 7-6 (7/4) huku Azarenka akimzidi mwenzake Laura siegemund kwa seti za 6-2, 6-2.
Bingwa huyo wa zamani sasa anaratibiwa kumenyana na Iga Swiatek raia wa Poland katika Raundi ya pili huku Danilovic akiratibiwa kumenyana na Linda Noskova wa taifa la Czech Republic.