News

ODM kuanza awamu ya pili ya uchaguzi wa mashinani

Published

on

Chama cha ODM kinatarajiwa kuanza awamu ya pili ya uchaguzi wake wa mashinani katika viwango vya wadi nchini.

Makamishna wa kamati kuu ya uchaguzi wa chama hicho, wakiongozwa na Mwenyekiti wao Emily Awita wameasema uchaguzi huo utajumuisha waliochaguliwa mwezi Novemba mwaka jana wa 2024.

Kulingana na taarifa yao, kamati hiyo imeeleza kuridhishwa na utayari wa shughuli hiyo ikisema uchaguzi huo utatekelezwa bila changamoto zozote.

Awita amesema washirikishi wote wa uchaguzi huo kote nchini wako tayari kusaidia kufanikisha zoezi hilo ambalo limeanza.

Zoezi hilo ambalo linatarajiwa kuendelea katika wadi zote isipokuwa maeneo machache ambayo uchaguzi huo ulisitishwa kwa muda huku awamu ya tatu ikitarajiwa kufanyika siku ya Jumatano wiki hii kwenye maeneo bunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version