News

Noor: Usalama Umeimarishwa Mombasa

Published

on

Kamishna wa kaunti ya Mombasa Mohammed Noor Hassan amewahakikishia wakaazi wa kaunti hiyo pamoja na watalii wanaolenga kuzuru mjini Mombasa kwamba usalama umeimarishwa hata wakati wa sherehe za Pasaka.

Akizunguza na Wanahabari mjini Mombasa, Noor amesema asasi za usalama katika kaunti hiyo zimeweka mikakati ya kushika doria mchana na usiku ili kudumisha usalama.

Aidha amekiri kwamba kitendo cha wizi wa simu ya mtalii mmoja mjini Mombasa wamebaini kwamba kilitekelezwa na kijana mmoja wa familia zinazo randa randa mitaani.

Wakati huo huo ameweka wazi kwamba kuna mikakati kabambe wanayolenga kuitekeleza ili kuhakikisha familia hizo zinadhibitiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version