Baraza la Magavana nchini limetishia kususia vikao vya kamati ya bunge la Seneti kuhusu hesabu za umma, likidai kwamba kumekuwa na vitendo vya uladhalilishaji, ulaghai wa kifedha na unyanyasaji dhidi ya magavana.
Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Gavana wa Wajir Ahmed Abdillahi, alisema baadhi ya maseneta kwenye kamati hiyo wamekuwa wakiwashambilia magavana kwa kisingizio cha kuuliza maswali pindi wanapofika mbele ya kamati hiyo.
Akisoma taarifa ya pamoja ya magavana hao baada ya kufanya kikao cha mazungumzo mjini Kilifi, magavana walisema hawatahudhuria vikao hivyo hadi masuala tata yatakapotatuliwa kati ya viongozi wa bunge la Seneti na baraza la magavana nchini.
Aidha gavana hao walishikilia kwamba iwapo watalazimika kufika mbele ya makamati mbalimbali za bunge la seneti kuelezea matumizi ya rasilimali za umma basi watafanya hivyo mara moja kwa kila roba ya mwaka.
Katika kikao hiyo Naibu Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Gavana wa Tharaka Nithi Mothomi Njuki aliwalaumu baadhi ya maseneti kwenye kamati hizo, akisema ndio chanzo cha masaibu hayo.
Taarifa ya Elizabeth Mwende
