Gachagua asema serikali ina njama ya kumuangamza

Gachagua asema serikali ina njama ya kumuangamza

Kinara wa Chama cha DCP Rigathi Gachagua amejitokeza na kudai kwamba serikali iko na njama ya kumuangamiza licha ya Rais William Ruto pamoja na wabunge kufualu kumtimua uongozini wakati akiwa Naibu Rais wa Kenya.

Gachagua alimshtumu Rais Ruto kutokana na uvamizi uliyotekelezwa wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisani la Witima eneo la Othaya kaunti ya Nyeri mapema leo asubuhi Januari, 25.

Gachagua aliweka wazi kwamba na watu anaodai kuwa maafisa wa polisi ambao hakuwa na sare za kazi ndio walitekeleza uvamizi huo, akisema walikuwa na njama ya kumuangamiza kwani matukio hayo yamekuwa yakiendelea mara kwa mara licha ya kuwasilisha ripoti wa idara ya upelelezi nchini DCI.

Katika kikao na Wanahabari nyumbani kwake katika eneo la Wamunyoro baada ya tukio hilo, Gachagua alimshtumu Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen, akisema agizo lake la uchunguzi kuhusu tukio hilo ni sawa na kuzima macho wakenya.

Kiongozi huyo hata hivyo alidokeza kwamba kuna mbunge mmoja pamoja na mkewe wamekuwa wakishirikiana na wakuu wa usalama kumfuatilia katika shughuli zake pamoja na kuvuruga mikutano yake ya kisiasa, akisema mbunge huyo yuko na malengo fiche.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi