Kaimu Spika wa bunge la kaunti ya Taita taveta Anselm Mwadime pamoja na wajumbe wengine wa bunge la kaunti hiyo wamewasilisha hoja yao mbele ya bunge la kitaifa
Anselm pamoja na Mwakilishi wadi wa Wundanyi Jimmy Mwamidi na Mwakilishi wadi mteule Shingira Rose, wanataka suala la usimamizi wa mbuga ya Wanyamapori ya Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi kusimamiwa na kaunt ya Taita taveta.
Bunge la kaunti ya Taita taveta linasema raslimali hiyo inafaa kuwa chini ya usimamizi wa serikali ya kaunti ya Taita taveta jinsi mbuga ya Wanyamapori ya Amboseli ilivyokabidhiwa serikali ya kaunti ya Kajiado.
Viongozi hao waliwasilisha hoja hiyo mbele ya kamati ya kitaifa kuhusu masuala ya umma wakitaka kubadilishwa hadhi ya mbuga ya wanyamapori ya Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi, wakisema mbuga hiyo inapatikana katika kaunti ya Taita taveta.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
